Kadi za harusi za kidijitali Tanzania
Tuma kadi za harusi kwa kila mgeni kwa WhatsApp na SMS, ujue nani amethibitisha kuja, na uscan kadi zao pindi watakapofika ukumbini. Sisi tunafanya kila kitu, wewe furahia sherehe.
Kwanini watu hawatumi mialiko ya harusi tena, kwa kadi za karatasi?
Kadi za karatasi ni ghali, zinachelewa kufika, na zinapotea. Hapa kwetu karibu kila mtu yupo WhatsApp, kwa hiyo kadi ikitumwa kwenye simu inamfikia mgeni papo hapo na wewe unajua nani ameipata. Hakuna kuprint, hakuna kuhangaika ukijiuliza kama kadi ilimfikia mtu au la.
Kinachotutofautisha Mialiko ni kwamba hatukuachii kazi. Hutakaa kudesign kadi wala kutuma ujumbe mmoja mmoja. Wewe tupe taarifa, sisi tunadesign, tunatuma kwa kila mgeni, na siku ya harusi tunakusaidia ukumbini.
Tunavyofanya kazi
Kuanzia orodha ya wageni mpaka siku ya harusi, hatua tano tu.
Tupe taarifa na orodha ya wageni
Tuambie majina ya bwana na bibi harusi, tarehe, na ukumbi, kisha utupe orodha ya wageni. Huhitaji account wala app.
Tunadesign kadi yako
Timu yetu inadesign kadi ya harusi yako, na kila mgeni anapata kadi yenye jina lake na QR code yake.
Tunatuma kwa kila mgeni
Kila mgeni anapata kadi yake kwa WhatsApp. Asiye na WhatsApp anaipata kwa SMS, hakuna anayeachwa.
Unajua nani anakuja
Majibu yanaingia kwenye dashboard yako moja kwa moja. Unaona nani amekubali, nani amekataa, na nani bado hajajibu.
Unascan kadi wanapofika ukumbini
Siku ya harusi, unascan kadi ya kila mgeni anapofika ukumbini. Kwa harusi inayofanyika Tanzania, timu yetu inaweza kuja kukufanyia kazi hiyo.
Tools za bure za kupanga harusi
Anza kupanga leo, bila kujisajili.
Excel ya orodha ya wageni
Fomu tayari ya kuandika majina, namba za simu, na idadi ya watu.
Download fomuMaswali kuhusu kadi za harusi za kidijitali
Maswali ambayo watu hutuuliza kabla ya kuanza.
Hukupata unachotafuta? Wasiliana na timu yetu
